Friday, April 17, 2009

SANDUKU LA AGANO LIKO WAPI?


Huu ni mfano wa sanduku la agano ambalo wana wa Israel waliambiwa watengeneze na Mussa wakiwa nyikani wakitoka Egypt (Misri) wakielekea promised land (Nchi ya ahadi). Sanduku hilo lilikuwa ni kama box la mbao lililotengenezwa na aina moja ya mbao inayoitwa (acacia wood) iliyofunikwa na dhahabu. Lilikuwa la urefu wa 1.15 metres, upana wa 0.7 metres na kimo cha 0.7 metres. Ilikuwa inabebwa na mishikio miwili mirefu ambayo ilikuwa imetengenezwa kwa mbao hiyo ya acasia ambazo pia zilikuwa zimefunikwa na dhahabu. Juu ya sanduku kuliwekwa makerubi wawili waliokuwa wamegeukiana mabawa yao yakiwa yamegusana. Uwepo wa Mungu haukuwepo ndani ya sanduku bali ulikuwa juu yake katikati ya hao makerubi. Uwepo wa Mungu juu ya sanduku hilo ulikuwa kama nuru. Kuhani mkuu alipaswa kufunika macho asiione nuru hiyo ("hakuna mwanadamu anionaye na akaishi" Kutoka 33 : 20) kila alipokuwa akiingia lilipokuwa sanduku ambapo ni patakatifu pa patakatifu. Hapa ndipo ambapo Mungu alipokuwa akiionana na Musa. Sanduku hili lilikuwa likibebwa na wana wa Walawi pekeyake hakuna mwingine aliyeruhusiwa kulishika, yeyote aliyedhubutu kulishika pasiporuhusiwa alikufa papohapo. Hao makerubi wawili wanawakilisha utukufu wa Mungu. Ndani ya sanduku hili kulikuwa na:


  1. Mawe mawili yaliyokuwa yameandikwa amri kumi za Mungu

  2. Fimbo ya Aron iliyoota mauwa

  3. Chombo cha dhahabu kilichokuwa na manna waliyokula wana wa Israel nyikani


Sanduku hilo lilikuwa linakaa patakatifu pa patakatifu, chumba cha ndani kabisa katika hema la kukutania. Aliyekuwa anaruhusiwa kuingia mahala hapo lilipokuwa sanduku hilo ni kuhani mkuu na alikuwa anaruhusiwa kuingia mara moja kwa mwaka. Kabla ya Kuhani mkuu kuingia patakatifu pa patakatifu alikuwa ni lazima aingie na damu ya mwana kondoo kwa niaba ya dhambi zake yeye mwenyewe na dhambi za wana wa Israel.


Sanduku la agano lilikuwa ndani ya hekalu lililojengwa na Solomon mpaka hekalu hilo lilipokujwa kuvunjwa mikononi mwa utawala wa Babylon ukioongozwa na Nebuchadnezzar. Kilichotokea kwa sanduku hilo hakijulikani ingawa haiwezekani kuwa lilichukuliwa na majeshi ya Babylon kama vilivyochukuliwa vyombo vingine vya hekalu kwasababu katika list ya vitu walivyovichukua sanduku la agano halikutajwa. Kulingana na baadhi ya vyanzo vya habari inasemekana kuwa mfalme Josiah, mmojawapo wa wafalme wa mwisho kutawala enzi za hekalu la kwanza, kutokana na unabii uliokuwa umetolewa alijua kuwa Jerusalem itavamiwa na Babylon, akalificha sanduku la agano. Alipolificha sanduku imekuwa kitendawili. Chanzo kingine cha habari kinasema kuwa mfalme Solomon alionyeshwa kuwa Hekalu litakujwa kuvunjwa na majeshi ya Babylon, kwahiyo akaandaa pango karibu na bahari ya shamu (dead sea) ambapo Josiah akaja kulificha sanduku. Na pia inasemekana nabii Yeremia (Jeremiah) alilificha sanduku chini ya Hekalu lililojengwa na Solomon. Na hata kuna tetesi ya kuwa hapa Tanzania kwenye misitu ya monduli kuna chombo chenye mfano wa sanduku la agano, ambacho kiliachwa hapo na majeshi ya Ujerumani enzi za ukoloni. Inasemekana kuwa chombo hicho kina miujiza na mambo mengi ya ajabu na kutisha.


Je wewe mdau unasemaje kuhusu chombo hiki cha jabu? Kwa mtazamo wako unadhani kipo wapi? Toa mchango wako kuhusu chombo hiki cha ajabu na kihistoria.

25 comments:

Unknown said...

Ninaomba kujua mtu aliyeliiba hilo Sanduku la agano

Unknown said...

Ukifuatilia habari hiyo ndugu ni kwamba Josia ndite alilolichukua

Unknown said...

Kutendawili

Festo sindani said...

Hiki chombo au sanduku hill yawezekan ndohilo la monduli labda MUNGU aliamua kulificha Tanzania kwetu na ndio maana tumekua nchi ya amani

Unknown said...

Mungu mwema yawezekana Tanzania tumepewa ilo sandaku

Wingu La Mashahidi said...

Kufahamu SANDUKU hili linafunua nini agano jipya bofya link hii >>> https://wingulamashahidi.org/maswali-yaliyoulizwa-na-majibu-yake/#qe-faq-1084

Unknown said...

Kweli pale monduli nilishafika na kusikia wakiekeza ule msitu wa juu ipo sanduku la maajabu sana

Unknown said...


Hilo sanduku la monduli wamelipiga picha?

Unknown said...

Tutubu sanduku lipo mbinguni UFUNUO WA YOHANA 11:15
UFUNUO WA YOHANA 11:19

Unknown said...

Sanduku halipo mbinguni. Musa alitengeneza hema ya kukutania kwa mfano wa ile hekalu ya mbinguni. Hata sanduku la agano lilionekana katika yale aliyooneshwa Musa. Waebrania 8:5

Unknown said...

Ufunuo wa yohana 11:15-19

Unknown said...

Soma vizur hiyo ufunuo mm nimeielewa iko sahih

Unknown said...


Unamanisha lilipaa au ilikuwaje make hapa tunaona vitu. Vingne vilichukuliwa na nebkandreza

Anonymous said...

Hakuna lililositirika ambalo halitafichuliwa

Anonymous said...

Dah Mimi nashindwa kuelewa kabisa

Anonymous said...

Lipo mwazyee kwetuuu

Anonymous said...

Amina

Anonymous said...

Sanduku la agano ukisoma ufunuo ni kwamba lipo mbinguni sasa

Anonymous said...

Sanduku hilo lilikua na maana kipindi hicho lakini kwasasa halina maana sababu sanduku halisi ni moyo wako. Ndani ya sanduku mlikua vitu 3 ambayo vinatakiwa viwe ndani yetu.
1.vibao vya sheria= inatakiwa sheria ya Mungu inae ndani yako
2.mana= neno la Mungu likae ndani yako.
3.kopo la dhahabu=ufalme wa Mungu ukae ndani yako.
Kwaiyo hilo sanduku hata ukilitapa halita kusaidia kitu. Mungu awabariki sana


Anonymous said...

mh kila agizo la mungu Lina maana Ufunuo 11:19 umeeleza Sanduku la agano liko mbinguni. saivi tu wadhambi Sana hatuwezi staimili utukufu wa mungu unao jidhihilisha katika Sanduku la agano ndio maana zamani ilikuwa anaelisogelea Hilo Sanduku la agano ni kuhani mkuu aliye aminiwa na mungu Napo lazima kuhani huyo awe amejitakasa ndio Aingie katika chumba kilicho na sanduku la agano. kwa Mimi siwezi stahimili utukufu wa Sanduku la agano maana kulitazama Tu nitakufa...

Anonymous said...

mh kila agizo la mungu Lina maana Ufunuo 11:19 umeeleza Sanduku la agano liko mbinguni. saivi tu wadhambi Sana hatuwezi staimili utukufu wa mungu unao jidhihilisha katika Sanduku la agano ndio maana zamani ilikuwa anaelisogelea Hilo Sanduku la agano ni kuhani mkuu aliye aminiwa na mungu Napo lazima kuhani huyo awe amejitakasa ndio Aingie katika chumba kilicho na sanduku la agano. kwa Mimi siwezi stahimili utukufu wa Sanduku la agano maana kulitazama Tu nitakufa...

Reply

Anonymous said...

Wazungu wametukaliliaha uongo kuwa ukweli wameichakachua bibilia yeti ya kikushi ya grazanes ya Ethiopia inakila kitu

Anonymous said...

Kiukweli mm Leo NAONA KUWA sanduku la Agano ni Biblia tu

Anonymous said...

Je hawako wale wafilisti wenye walikuwa wakilitafuta njo wenye walio lichukuwa?

Anonymous said...

Nahis hiv saduku la agano lipo maka ambapo waisilam huenda kuhij Kila mwaka