Monday, March 30, 2009

HUYU NI MALAIKA?


Picha hii ilichukuliwa na mwanamke mmoja kwenye state ya Colorado, U.S.A. Ilipigwa wakati wa mashindano ya kupiga picha nyota ambayo walishiriki watu wapatao 150. Mwanamke huyo alitumia camera maalum iliyo na uwezo mkubwa wa kuona mbali kwenye anga na akapiga picha nyota za anga. Bila kugundua ni kitu gani alichokipiga kwenye picha yake akaipeleka picha yake kwa developer. Developer alipoiona akamuuliza alipigaje hiyo picha na akamuuliza kama hajaona kitu chochote cha ajabu kwenye picha hiyo. Kwenye hiyo picha kimeonekana kitu kama kiumbe mfano wa malaika. Ukitazama vizuri utaona mabawa makubwa, kichwa na sura kama ya mwanamke akiwa amevaa taji (crown) la dhahabu likiwa limezungukwa na vito vya thamani, uso wake umegeuka upande, ukiangalia vizuri unaweza kuona sehemu ya jicho, pua, sikio na mdomo. Ukija chini utaona bega la kulia pamoja na mkono ambao sehemu kubwa yake umefunikwa na nyota. Wadau leteni maoni yenu hiki ni kitu gani? Je huyu mwanamke alimpiga picha malaika bila kujua? au pepo (jini)?. Nigependa kupata maoni yako kuhusiana na picha hii.

1 comment:

Anonymous said...

I own this picture. I was told it was not “good”
Possibly jinn .
But I’m not convinced