Wednesday, April 1, 2009

SAFINA YA NUHU (NOAH'S ARK) YAPATIKANA





"Safina ya Nuhu imepatikana katika mpaka wa Uturuki na Iran (Turkish-Iranian border) kilometre 32 kutoka mlima Ararat (Mount Ararat)" maneno hayo yalisemwa na kiongozi wa wanasayansi ambao wamekuwa wakifanya utafiti mahala hapo (site of the ark) kwa takribani miaka sita.


Serikali ya Uturuki (Turkish government) ilishawishika na unguduzi huo kiasi kwamba imeitenga sehemu hiyo (site of the ark) ipate kufanyiwa uchunguzi zaidi na imeruhusu uchimbaji wa eneo hilo ambao unatizamiwa kufanyika mwishoni wa mwaka huu wa 2009 ili utafiti wa kina kuhusiana na merikebu hiyo ufanyike.


Sehemu hiyo isiyokuwa na makazi ya watu (site of the ark), ina chombo chenye mfano wa boti au meli kubwa iliyozikwa chini juu juu chini (upside down) resting an altitude of 2,300 metres. Ikiwa na urefu wa mita 170 (170 metres) na upana wa mita 45 (45 metres), chombo hicho kwa vipimo kinalingana na vipimo vya Safina ambayo Mungu alimuagiza Nuhu kutengeza kama kitabu cha Mwanzo 6 (Genesis 6) kwenye Biblia kinavyosema.


Wanasayansi wa Marekani na Mashariki ya Kati wamegundua majiwe makubwa yakiwa na matundu upande wa mwisho wa merikebu hiyo, amabayo yanaaminika kuwa ni "drogue stones" yaliyo kuwa yakitumiwa kuifanya merikebu kuwa stable katika ulimwengu wa nyakati za zamani. Yalikuwa yakifungwa nyuma ya merikebu na kuvutwa.


Salih Bayraktutan, mkubwa wa kitengo cha geology katika chuo kikuu cha Uturuki Ataturk University kwa kupitia vipimo maalum amesema miaka ya chombo inasadikiwa kuwa ni zaidi ya 100,000 (100,000 years).


David fasold mtaalamu wa Kimarekani wa merikebu zilizozama (an American shipwrecked specialist) asiyekuwa na dini (Atheist) ambaye amekuwa akiongoza uchunguzi huo alisema "picha za radar zilizopiga maeneo hayo (site of the ark) zimetokea vizuri sana"


Lkini uchunguzi huo umewakwaza wakristo wengi ambao wamekuwa wakienda nchini Uturuki kutafuta mahala ambapo Safina hiyo ilipoishia wakiamini kuwa inapaswa kupatikana mlima Ararat (Mount Ararat).


Kuna ambao wanaamini kuwa chombo hicho ni Safina ya Nuhu iliyozungumziwa kwenye Biblia na Quran na wengine wanapinga kabisa kuwa siyo kila mtu kwa maoni yake kutokana na uelewa wake. Je wewe wasema nini kuhusiana na ufumbuzi huu? Je ni kweli unaamini kuwa Safina ya Nuhu imepatikana?


Mdau toa maoni yako kuhusiana na chombo hicho cha ajabu kilichogungulika huko mpakani mwa nchi ya Uturuki na Iran.


9 comments:

Anonymous said...

kwani NUHU alikuwa anaishi wapi? ila nafahamu kuwa meli yake ilielea hadi kwanye milima ila sijui ni mlima gani yawezekana ndo hiyo

Anonymous said...

inawezekana ikawa ni yenyewe tusubiri kuskia kutoka kwa archeologists wakishamaliza kazi yao kuichunguza

Anonymous said...

Nuhu jembe la mungu!!!!

Anonymous said...

alikuwa mtu muadilifu

Anonymous said...

but i think those ajust assumption no knows the exact how the ark look like

Anonymous said...

Hapo ndio inakuja utata kuhusu umri wa dunia hii.

Kibiblia umri wa dunia haufiki hata miaka 8,000. sasa hao watalaamu na na miaka 100,000 ya Safina, inakuwaje? Kweli ni utata.

Anonymous said...

Laundi hii lazima muamini kuwa mungu yupo2 na dunia INA miaka mingi siyo 8,000

Anonymous said...

Kumbuka siku Moja Kwa MUNGU n miaka 1,000 na neno linautaja mlima Ararat mwanzo 8:4

Anonymous said...

Wanasayansi wanataka kutawala dunia na wanaonekana kupinga sana vitu vya mwenyez mungu na asilimia nying wanaamini sayansi ila nashauli kuwa imara katika imani yako na usisikilize puuI za dunia